Sikufanya lolote baya kwa Trump – Global Publishers

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekataa kuomba msamaha baada ya mabishano makali na majibizano ya maneno na mwenzake wa Marekani, Donald Trump katika Ikulu ya White House. Mkutano wa viongozi hao wawili katika Ofisi ya Oval, ambao hapo awali ulipangwa kukamilisha makubaliano ya kuipatia Marekani haki ya madini adimu ya Ukraine, uligeuka…

Read More

Magari yagongana Moro, wawili wafariki

Morogoro. Watu wawili wamethibitika kufariki dunia papohapo katika tukio la ajiali lililohusisha magari mawili kugongana uso kwa uso na kuwaka moto katika eneo la nanenane Manispaa ya Morogoro barabara kuu ya Morogoro Dar es Salaam. Ajali hiyo imetokea saa saba usiku wa kuamkia leo Machi 04, 2025. Magari hayo mawili moja ni lori la mafuta…

Read More

TANZANIA YAVUNJA REKODI ONGEZEKO LA WANYAMAPORI

  Na Emmanuel Buhohela – Dodoma Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema ongezeko la idadi ya Wanyamapori katika hifadhi za Wanyama hapa nchini imetokana na juhudi za serikali kushirikisha wadau wa uhifadhi wa Wanyamapori na wananchi kwa ujumla hali iliyopelekea kukua kwa utalii na uchumi katika Taifa. Ameyasema hayo leo…

Read More

Fadlu aipata dawa ya Yanga | Mwanaspoti

HOMA ya pambano la Dabi ya Karikoo, imeanza kupanda mapema kwa mashabiki wa Simba na Yanga, kila mmoja akitamba kupta ushindi, japo wale wa Simba wanaonekana kuwa wanyonge mbele ya wenzao kutokana na kupoteza mechi nne mfululizo zilizopita katika mashindano tofauti. Hata hivyo, kocha mkuu wa Simba, Fadlu Davids ameshtukia jambo na fasta akawatoa hofu…

Read More

Nafuu kwa bajaj, magari yanayotumia gesi Dar

Dar es Salaam. Huenda sasa kilio cha foleni kwa wanaotumia vyombo vya moto vya gesi kikapungua kutokana na ongezeko la vituo vya kujazia gesi, wachambuzi wanasema manufaa si tu kwa kundi hilo. Matumizi ya gesi asilia kwenye magari kawaida huokoa gharama kwa zaidi ya asilimia 50 ikilinganishwa na dizeli na petroli. Kwanza, gesi huuzwa bei…

Read More

BENKI YA CRDB, UNDP zazindua programu kuwasaidia wafanyabiashara kufikia Soko Huru la Afrika (AfCTA)

Taasisi ya CRDB Bank Foundation (CBF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa (UNDP), leo wamezindua mwongozo uliorahisishwa kwa wajasiriamali wadogo na wa kati nchini wenye fursa za kuwaunganisha na Soko Huru la Afrika (AfCTA) utakao wawaongezea uwezo na maarifa zaidi ili waweze kupanua biashara zao kote barani Afrika. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo…

Read More

Kiwango cha Samatta PAOK moto!

KWA kiwango anachoonyesha Mbwana Samatta katika Klabu ya PAOK kule Ugiriki ni kama kinawapa mtihani viongozi kuamua hatima yake kutokana na mkataba wake kukaribia mwisho. Machi 2, mwaka huu, nahodha huyo wa Taifa Stas alifunga bao moja na asisti kwenye mechi ya raundi ya 25 dhidi ya Asteras Tripolis, PAOK ikiondoka na ushindi wa mabao…

Read More

Elimu yetu inaandaa watu wenye hekima na busara?

Tuanze na msemo huu wa Wamarekani wa asili ambao wazungu wa Ulaya waliwaita kimakosa kwa jina la Wahindi wekundu. Hawa wana msemo huu: ‘’Chochote utakachofanya angalia kitawaathiri vipi vizazi vinne vijavyo? Kwa mfano kama tunataka kufanya kilimo mahali fulani, au tunataka kujenga nyumba sehemu hiyo, au tunataka kujenga barabara itoke huku iende kule, tufikirie kwa…

Read More