
Makalla azusha tafrani, wadau wamkalia kooni
Dar es Salaam. Kauli yenye tuhuma iliyotolewa na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla imezusha sintofahamu huku wadau wakiwamo viongozi wa kisiasa wakimtaka ajitokeze kutoa ushahidi au aombe radhi. Juzi, Makalla akizungumza na wanachama wa CCM mkoani Simiyu, alitoa shutuma dhidi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia…