
Wajawazito Mwanza kushiriki marathoni, faida zatajwa
Mwanza. Wajawazito wametakiwa kushiriki mazoezi na mbio fupi ikielezwa kwamba yanasaidia kuimarisha mwili, mzunguko wa damu na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo presha, kisukari na kupunguza uzito. Ushauri huo umetolewa Machi 21, 2025 na Mratibu wa Huduma ya Afya ya Uzazi katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Bertha Yohana, akieleza kuwa kutokana na umuhimu wa wajawazito…