
Rea, Tanesco wapewa agizo hili bei za kuunganisha umeme
Njombe. Wakati uunganishwaji wa umeme katika maeneo ya vijiji ukiwa ni Sh27,000 na Sh320,960 mijini, Wakala wa Nishati Vijijini (Rea) na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wameagizwa kubandika gharama halisi za kuunganisha umeme katika ofisi za serikali za vijiji. Gharama hizo ziende sambamba na hatua ambazo mwananchi anapaswa kuzifuata akitaka kuunganishishiwa umeme ili wananchi wazifahamu…