Lissu afikishwa mahakamani Kisutu | Mwananchi

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Lissu amefikishwa mahakamani hapo leo Aprili 10, 2025 saa 10: 15 alasiri na kuwekwa kwenye mahabusu iliyopo mahakamani hapo.

Mwanasiasa huyo alikamatwa jana Aprili 9, 2025 wilayani Mbinga mkoani Ruvuma muda mfupi baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara na kusafirishwa hadi Dar es Salaam. Kabla ya kufikishwa mahakamani hapo, Lissu alihojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Central jijini Dar es Salaam.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi