NDEJEMBI AAGIZA KUBOMOLEWA NYUMBA ILIYOJENGWA ENEO LILILOVAMIWA
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi amemwelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuchukua hatua za haraka za kuvunja nyumba iliyojengwa katika kiwanja kikichovamiwa eneo la Iyumbu North mkoani Dodoma. Waziri Ndejembi ametoa agizo hilo April 16, 2025 alipotembelea eneo la kiwanja hicho namba 1/31 kilichopo Block D, Iyumbu…