
Kinje wa AAFP mguu sawa kinyang’anyiro urais 2025
Dar es Salaam. Chama cha siasa cha Wakulima (AAFP) leo kimemteua rasmi kada wake, Kunje Ngombale-Mwiru kuwa mgombea wa urais atakayewakilisha chama hicho katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu. Hata hivyo, chama hicho kimeshindwa kumpata mgombea urais upande wa Zanzibar baada ya aliyekuwa anawania nafasi hiyo, Said Soud kupigiwa kura nyingi za hapana….