
SIMULIZI ZA UCHUNGU NA MAPAMBANO YA HAKI: TANZANIA NA CHANGAMOTO ZA UTEKELEZAJI WA HAKI YA AFYA YA UZAZI KWA WAATHIRIKA WA UKATILI WA KIJINSIA
KATIKA kona nyingi za jamii yetu, simulizi za uchungu, maumivu na ukimya zimeendelea kuwasibu wanawake na wasichana wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia na kuishia kupata mimba zisizotarajiwa. Ukatili wa kijinsia si jambo geni tena. Wanawake wengi wameripotiwa kupigwa, kubakwa, kulazimishwa kufanya tendo la ndoa bila ridhaa yao, au hata kudhalilishwa kihisia. Haya yote huacha majeraha makubwa…