Hekima, busara nguzo muhimu kwa makuzi ya mtoto
Katika ulimwengu wa leo ambao umejaa vishawishi, mashinikizo na changamoto nyingi, hakuna zawadi bora ambayo mzazi anaweza kumpatia mtoto wake zaidi ya kumjengea msingi wa hekima na busara. Tunaambiwa kuwa hili ni jukumu lisiloisha na linahitaji subira, mawasiliano ya mara kwa mara na mfano wa kuigwa baina ya mzazi na mwanawe. Na tunaambiwa kwa kuwafundisha…