Mwili wa mwanamke wakutwa nje ya nyumba ukiwa mtupu
Unguja. Mwili wa mwanamke ambaye bado hajafahamika jina, umekutwa leo Aprili 12, 2025, saa 12 asubuhi nje ya jengo la Michenzani, Block namba nane, katika Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, ACP Abubakar Khamis Ally amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa uchunguzi wa awali umeonyesha…