
Waajiri wakumbushwa kujiweka tayari mabadiliko ya teknolojia
Dar es Salaam. Serikali imewakumbusha waajiri nchini kujiweka tayari kupokea mabadiliko ya teknolojia huku wakichukua tahadhari dhidi ya athari zake hasi zinazoweza kutokea ikiwemo upotevu wa baadhi ya fursa za ajira. Wito huo umetolewa Aprili 28, 2025 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete wakati akiwaongoza…