Mahakama yatoa uamuzi kesi ya uraia wa mastaa Singida BS
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imeitupa kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Wakili Peter Madeleka kupinga uamuzi wa Serikali kuwapa uraia wa Tanzania nyota watatu wa timu ya Singida Black Stars. Nyota hao ni Emmanuel Keyekeh, raia wa Ghana; Josephat Bada (Ivory Coast) na Muhamed Camara (Guinea). Uamuzi wa kuitupa kesi hiyo ulitolewa na Jaji Evaristo Longopa…