AKILI ZA KIJIWENI: Kwaheri KenGold mmevuna mlichokipanda
TATHMINI ya kimpira hapa kijiweni imeishusha rasmi daraja KenGold kutoka Ligi Kuu kwenda Ligi ya Championship japo imebakiwa na mechi nne mkononi ambazo ikishinda itapata pointi 12 na ikijumlisha na ilizonazo 16, jumla itakuwa na 28. Ukiangalia msimamo wa Ligi Kuu, kuna timu kama nne hivi ambazo zinahitaji pointi mbili tu katika michezo ambazo zimebakiza…