TLS: Kila hoja inayopigiwa kelele uchaguzi mkuu ina mantiki

Dar es Salaam. Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimeibeba ajenda ya uchaguzi mkuu mwaka huu ikieleza kila hoja inayopigiwa kelele na pande mbili zinazokinzana kuhusu uchaguzi huo ina mantiki. TLS imekwenda mbali zaidi na kueleza kuwakutanisha wadau wote wa uchaguzi ili kuwa na makubaliano ya pamoja, kabla ya kwenda kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba…

Read More

RC Chongolo kuondoa changamoto ya foleni ya malori Tunduma

Tunduma. Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo, ameunda kamati maalumu kuchunguza sababu za ucheleweshaji wa malori ya mizigo kuvuka mpaka wa Tunduma, ambapo imebainika baadhi hukaa hadi siku nane yakisubiri vibali vya kuvuka. Kamati hiyo imeundwa baada ya Chongolo kufanya mazungumzo na wadau wa usafirishaji kwenye kituo cha kutoa huduma kwa pamoja (OSBP) kilichopo…

Read More

Bei ya mchele Mbeya yapaa, Serikali yafafanua

Mbeya. Wakati bei ya mchele ikipanda mkoani Mbeya, wakulima wa zao hilo wamesema huenda bidhaa hiyo ikazidi kupanda kutokana na ukame wa mvua msimu huu. Kwa sasa bei ya zao hilo ipo juu ambapo ndoo ya kilo 20 imefikia kati ya Sh60,000 hadi Sh65,000 kutokana na ubora sokoni, hali inayotia hofu kwa wananchi haswa wenye…

Read More

Lissu adaiwa kushikiliwa na Polisi Ruvuma

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu anadaiwa kushirikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma muda mchache baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Mbinga mkoani humo. Bado haijafahamika chanzo cha Lissu, pamoja na walinzi wake wawili, kada mmoja wa chama aliyefahamika kama Shija Shebeshi kushikiliwa na polisi,…

Read More

BoT yataja maeneo ya kumwezesha mwanamke kiuchumi

Dar es Salaam. Ili kuharakisha ujumuishaji wa kifedha kwa wanawake, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetaja maeneo ambayo yanapaswa kuwekewa mkazo zaidi ikiwemo kurahisisha upatikanaji wa mitaji kwao. Maeneo mengine ni elimu ya kifedha na uwezeshaji, kuwepo kwa sera na utetezi hasa zinazochochea usawa wa kijinsia katika sekta ya kifedha. Hayo yamesemwa na Naibu Gavana…

Read More

Afariki dunia baada ya kujirusha chini ya uvungu wa gari

Kahama. Mwanaume ambaye jina lake halikufahamika, amefariki dunia baada ya kujirusha chini ya uvungu wa gari la mizigo, mali ya kampuni ya CIMC. Ajali hiyo ilitokea kwenye barabara kuu ya Kahama kuelekea Masumbwe, wilayani Kahama, mkoani Shinyanga, Aprili 7, 2025. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi, alithibitisha tukio hilo na kusema kwamba…

Read More

Pombe, sigara chanzo watoto kukosa ubongo, mimba kuharibika

Mbeya. Wajawazito wanaotumia vilevi na sigara kupita kiasi, wako hatarini kupata watoto wasio na ubongo ‘alcoholic syndrome’ tatizo linalosababisha ubongo wa mtoto kutofanya kazi, kutokomaa maumbile na tundu kwenye moyo. Madhara mengine ni kujifungua watoto wenye changamoto mbalimbali wakiwepo  njiti, kuzaliwa na changamoto  ya vichwa vikubwa, mgongo wazi hususani kwa  mjamzito mimba kuharibika ikiwa chini…

Read More

Wanaodaiwa kutapeli wastaafu, waendelea kusota rumande

Dar es Salaam. Serikali imedai upelelezi wa kesi ya kutumia laini ya simu iliyosajiliwa kwa jina la mtu mwingine na kutapeli wastaafu, inayowakabili wakazi wanne wa Kagera na Mwanza, bado haujakamilika. Washtakiwa katika kesi hiyo ni Eradius Rwechungura (43) maarufu Rwamakala na mkazi wa Kiseke- Mwanza; Heri Kabaju (37), maarufu Babylon ambaye ni mchuuzi wa…

Read More

Ewura kufanya tathmini bei ya umeme

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Dk James Mwainyekule amesema katika mwaka wa fedha ujao 2025/2026 wanakusudia kufanya utafiti kuhusiana na gharama halisi za utoaji wa huduma za umeme. Hili linafanyika baada ya kukamilishwa kwa miradi mikubwa ya umeme iliyofanywa na Serikali, ikiwemo ule wa…

Read More