Serikali yaja na ahadi nyingine ujio wa mabasi ya mwendokasi
Dar es Salaam. Ahadi nyingine imetolewa kuhusu ujio wa mabasi ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT), ikiwa ni ahadi ya tatu kutolewa tangu mwaka huu uanze. Katika ahadi hii, kwa mujibu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), jumla ya mabasi 755 yanatarajiwa kuwasili kati ya Mei na Juni, 2025 na yatatoa huduma katika…