VIDEO: Wananchi wapewa mbinu kukabiliana na polisi wanaokamata watu ‘kihuni’
Geita. Jeshi la Polisi mkoani Geita limetoa wito kwa wananchi kutokubali kukamatwa na mtu yeyote anayejitambulisha kama askari polisi bila kuonyesha kitambulisho cha utumishi na kueleza kituo cha polisi alichotoka. Jeshi hilo limesema kitendo cha kutokuonyesha kitambulisho au kituo cha kazi ni kinyume cha sheria na kinaweza kutumika kama mbinu ya kuficha vitendo vya kihalifu….