Dk Nchimbi alivyohitimisha ziara nyumbani kwao

Ruvuma. Ziara ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi mkoani Ruvuma imetamatika, huku akisisitiza wananchi kujiandaa kwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 pamoja na kuilinda amani ya nchi. Mbali na hilo, amesema chama hicho kitaendelea kupambana usiku na mchana kuhakikisha inatatua changamoto za wananchi na kuwapelekea maendeleo ili kuchagiza ustawi wa…

Read More

Rais Samia kuhutubia Bunge Angola

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kulihutubia Bunge la Angola ikiwamo kufanya mazungumzo na Rais  João Lourenço wa nchi hiyo. Rais Samia ambaye anaanza ziara ya siku tatu nchini humo kuanzia Aprili 7 hadi Aprili 9, 2025, mbali na kulihutubia Bunge pia ataweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu wa muasisi wa…

Read More

TANZANIA YAJIANDAA NA KONGAMANO KUBWA LA USALAMA MTANDAONI

 ***** Katika hali ya kuendelea kuongezeka kwa vitisho vya kimtandao duniani, Tanzania inaendelea kuchukua hatua madhubuti za kulinda miundombinu yake ya kidijitali.  Nchi hiyo itafanya Kongamano kubwa la Usalama Mtandaoni kuanzia Aprili 10, 2025, katika Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.  Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika kwa siku mbili na linadhihirisha dhamira ya Tanzania kuimarisha uimara…

Read More

Sendiga aagiza polisi kata awekwe rumande kwa uzembe

Simanjiro. Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, amemuagiza Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Simanjiro, Kidwadi Ally kumlaza mahabusu polisi wa Kata ya Loiborsiret, Ester Tairo kwa uzembe wa kushindwa kumchukulia hatua mtu aliyempa mimba mwanafunzi wa shule ya sekondari. Pia, Sendiga amemweleza Ally, kuwa askari polisi wa eneo hilo wanalalamikiwa kwa kupokea rushwa,…

Read More

Mvua yafunga barabara Somanga-Mtama | Mwananchi

Lindi. Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Lindi, umesitisha matumizi ya barabara ya Somanga-Mtama kwa muda baada ya mafuriko yaliyosababishwa na mvua zilizonyesha wilayani Kilwa, mkoani hapa. Akizungumzia hilo leo Jumapili Aprili 6, 2025, Meneja wa Tanroads Mkoa wa Lindi, Emil Zengo amesema wamelazimika kuifunga baada ya maji kujaa kiasi cha barabara kushinda kupitika….

Read More

Wadau: Ushuru mpya wa Trump, uiamshe Tanzania

Dar es Salaam. Kuimarisha diplomasia ya kiuchumi na kushirikiana na mataifa yaliyo tayari, kama vile China ni miongoni mwa ushauri uliotolewa na wataalamu wa uchumi nchini Tanzania. Ushauri huo ulitolewa kwa nyakati tofauti na maprofesa wa uchumi, Ibrahim Lipumba na Anna Tibaijuka, pamoja na Mbunge wa Bumbuli na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na…

Read More

Mbege, kiburu vyatajwa kuimarisha kinga ya mwili

Dar/Moshi. Majaribio ya utafiti wa kisayansi, yamebaini mbege na vyakula vya asili, kikiwamo kiburu vina faida kubwa katika uimarishaji kinga ya mwili kwa mwanaume. Kiburu ni chakula cha asili cha jamii ya Wachanga ambacho hupikwa kwenye chungu kwa kuchanganya maharage, ndizi na viungo kama nyanya na kitunguu. Mbege ni kinywaji kinachotengenezwa kwa kutumia ndizi mbivu,…

Read More

Ang’atwa na kunyofolewa mdomo na mchepuko wake

Kakamega. Mkazi wa Kakamega, Douglas Shisia amejikuta  katika maumivu baada ya kung’atwa na kunyofolewa mdomo na mwanamke aliyetajwa kuwa ni mchepuko wake, alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake. Shisia (45) ambaye anaishi Nairobi na familia yake akiwamo mkewe na watoto, alisafiri hadi Shiatsala Kakamega, anapoishi mchepuko huyo ambaye jina lake halikufahamika Jumatano Aprili 2, 2025 kwa lengo…

Read More