Kauli ya atabadilika inavyowaponza wanandoa

Uhusiano wa kimapenzi, ni sehemu muhimu ya maisha ya kila mtu. Mara nyingi, watu wanatarajia kuwa na wenza wanaoendana nao katika mawazo, mitindo ya maisha na maadili. Hata hivyo, wakati mwingine mtu anaweza kuingia katika uhusiano na mtu mwenye tabia mbaya, akiamini kuwa atakuwa na uwezo wa kumbadilisha au kumwongoza ili kuboresha tabia hizo.  Kuna…

Read More

Madhara ya watu wazima kutegemea wazazi kiuchumi

Kutegemea wazazi kiuchumi wakati mtu ameshakuwa mtu mzima kunaweza kuwa na madhara makubwa kwa maisha ya mtu binafsi, familia, na hata jamii kwa ujumla. Ingawa kuna hali zinazolazimisha baadhi ya watu kuendelea kutegemea wazazi, kama ugonjwa au ukosefu wa ajira, kuwa tegemezi kwa muda mrefu kunaweza kuathiri maendeleo ya mtu binafsi na mfumo wa kifamilia….

Read More

Hakuna mtoto anayezaliwa na ukorofi

Juzi nimepokea taarifa za kusikitisha. Baraka mtoto wa jirani yetu enzi hizo amekuwa kilema. Jicho lake moja limeng’olewa, hana mkono moja, uso umejawa makovu shauri ya vipigo vya ‘wananchi wenye hasira kali.’ Sikushangaa kusikia Baraka anadaiwa kuwa jambazi sugu, anayetishia usalama wa watu na mali zao.  Inadaiwa, kwa miaka mingi tangu awe mtu mzima, Baraka…

Read More

Mzazi fanya haya kumsaidia mwanao kuhimili hisia kali

Katika safari ya maisha, watoto hukumbana na changamoto mbalimbali zinazoweza kuwafanya wapitie hisia kali kama hasira, huzuni, hofu, au msongo wa mawazo. Hisia hizi zisipodhibitiwa mapema, zinaweza kuwa na athari mbaya katika maendeleo yao ya baadaye. Hivyo wazazi wana nafasi muhimu katika kuwasaidia watoto wao kujifunza jinsi ya kudhibiti hisia kali na kuzielekeza katika njia…

Read More

Mapenzi ni hatua tano, wewe uko ya ngapi?

“Inawezekana hakuwa wa kwangu. Yumkini Mungu hakupanga tuwe pamoja. Labda Mungu ameniepushia mengi”. Mara kwa mara wengi tumesikia sentensi zinazofanana na hizi hususani kwenye vinywa vya watu, marafiki au ndugu zetu ambao wamewahi kuachana, kutengana au kuvunja uhusiano. Tafiti za kisaikolojia kwenye eneo la uhusiano pamoja na yale mengi tunayokutana nayo tunapowashauri wapenzi na wanandoa…

Read More

Haya ndiyo machungu wanayopitia wanawake maishani

Acha niwape ‘story’ ya yanayomsibu mwanamke. Ninapogombana na mwanaume, anaponipiga makofi, kunikata na visu, kunipiga na mabapa ya panga hata kunitishia kunichoma na bisibisi, dunia nzima itanishikia kiuno. Wengi wakiwamo wanawake wenzangu watanyanyua midomo yao juu kama chuchunge bila kujua ninachopitia na mahakimu wasiosomea watatoa hukumu zao kwamba mimi ndio tatizo na kwa yaliyonikuta ni…

Read More

Umuhimu wa wanandoa kutunza siri

Kuna busara wakati wa kuwafunda wanawali katika jamii moja nchini Uganda isemayo kuwa wanapoolewa lazima wajifunze kufunga miguu na kufungua macho badala ya kufungua miguu na kufunga macho. Hii hufanyika wakati mwali akijiandaa kwenda kwa mumewe. Wazazi hufanya hivyo kwa kujua kuwa nyumbani kwa mwali huacha kuwa kwao na huko aendako ndiko hugeuka kwake. Hamjasikia…

Read More

Matibabu ya wastaafu NHIF yazua mgongano -3

Dar es Salaam. Ni mgongano wa masilahi, ndivyo inavyodhihiri katika huduma ya matibabu kati ya kundi la wazee wastaafu na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF). Wakati wazee wakisisitiza wanastahili kuendelea kutibiwa bure kwa kuwa walichangia kwa miaka mingi wakati wa ajira zao, NHIF inapendekeza waanze kuchangia sehemu ya matibabu kutoka kwenye pensheni…

Read More