ANTI BETTY: Nimwambie shemeji watoto anaolea sio wake?
Anti habari. Naomba usiniwashie moto nisaidie nifanyeje kutoa au kuishi na siri hii maana naona imeanza kunishinda. Nina rafiki yangu wa tangu shule ya awali, tulipoteana baadaye nikaja kukutana naye baada ya mume wangu na wake kuwa wanafanya kazi ofisi moja. Kwa kuwa tulikuwa marafiki kuanzia hapo tukawa karibu zaidi. Sasa hivi ana watoto watatu,…