Chadema kinawaka, watia nia njia panda
Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewaweka njiapanda watia nia katika uchaguzi mkuu ujao baada ya kusisitiza msimamo wake wa hakuna mabadiliko, hakuna uchaguzi kushinikiza mifumo ya uchaguzi kurekebishwa. Watia nia wa ubunge na udiwani wametakiwa kuchagua ama kukihama chama hicho kwenda kugombea kupitia vyama vingine au kuungana na viongozi kupigania mabadiliko…