Shambulizi la Russia laua wanne Ukraine, 16 wajeruhiwa

Kyiv. Jeshi la Russia limetekeleza mashambulizi ya anga kwa kutumia ndege zisizo na rubani (droni) na kombola la ‘balistiki’ katika Mji wa Kryvyri nchini Ukraine na kusababisha vifo vya watu wanne, huku 14 wakijeruhiwa. Shirika la habari la Associated Press limeripoti kuwa mashambulizi hayo ya Russia nchini Ukraine yametekelezwa usiku kucha wa kuamkia leo Alhamisi…

Read More

Saba wafariki dunia ajali ya basi Mwanga, 32 wajeruhiwa

Mwanga. Watu Saba wamefariki dunia papo hapo huku wengine 32 wakijeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Mvungi, walilokuwa wakisafiria kupinduka katika eneo la Kijiji cha Mamba, Kata ya Msangeni, Tarafa ya Ugweno, Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro. Kamanda ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo,  ambapo…

Read More

Umuhimu wa kuachanisha uzao mmoja na mwingine

Zimebaki  siku chache ili kuadhimisha siku ya Afya Duniani ambayo inaadhimishwa kila mwaka tarehe 7 Aprili chini ya mwamvuli wa Shirika la Afya Duniani (WHO).  Kampeni ya siku hii kwa mwaka huu inaangazia afya ya uzazi na watoto, na kuzitaka serikali na jumuiya ya afya duniani kuimarisha juhudi za kukomesha vifo vinavyoweza kuzuilika vya uzazi…

Read More

AKILI ZA KIJIWENI: Ateba abadilike Simba inamtegemea

JANA Lionel Ateba katukwaza sana hapa kijiweni baada ya mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baina ya Al Masry na Simba uliochezwa kule Misri. Kulikuwa na makundi mawili yaliyotibuliwa nyongo na Ateba mara baada ya mechi hiyo iliyomalizika kwa Simba kufungwa mabao 2-0 ambayo tuliitazama kwa pamoja katika banda la…

Read More

Abaya la Eid, Iinafundisha katika maisha ya kiuchumi

Siku zote kadiri Sikukuu ya Eid inavyokaribia, ndivyo hamasa za manunuzi ya nguo mpya inavyoongezeka. Kwa wanawake, hakikisho kubwa ni kutopitwa na abaya mpya, neno ambalo limepata umaarufu mkubwa likimaanisha vazi la buibui, mavazi ya heshima yanayovaliwa na wanawake wa dini ya Kiislamu. Mbali na kuwa sehemu ya utambulisho wa kitamaduni na dini, ununuzi wa…

Read More

Tanzania kinara uwekezaji nchini Kenya

Huenda ikawa ni jambo la kushangaza kwa wengi, lakini ukweli usiopingika ni kwamba Tanzania inaongoza katika uwekezaji nchini Kenya, licha ya kuwa nayo bado inaendelea kutafuta fursa zaidi za kuvutia wawekezaji wa ndani na wa kimataifa ili kukuza uchumi wake. Serikali ya Tanzania imekuwa ikiweka mikakati mbalimbali ya kuboresha mazingira ya biashara, ikiwa ni pamoja…

Read More

Sababu bidhaa nyingi za nje kupita kanda ya ziwa

Kutokana na uwepo wa bandari katika kanda ya Dar es Salaam, Kanda ya Kaskazini, na Kanda ya kusini Mashariki, kunaweza kukufanya ufikiri tofauti, lakini takwimu zimeonyesha uhalisia. Ripoti ya Uchumi wa Kikanda ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa robo ya mwaka iliyoishia Septemba 2024, Kanda ya Ziwa imeongoza kwa kusafirisha bidhaa kwenda nje ya…

Read More

Njia za kulinda mtaji katika biashara yako

Katika biashara kunakuwa na mtaji wa muda mrefu ambao unashikilia msingi wa biashara yako ya mahitaji ya kifedha ya muda mrefu na mtaji wa uendeshaji wa biashara ambao unaweza kuongezeka au kupungua kutokana na namna ambavyo unaendesha biashara yako. Mtaji wa muda mrefu ni ule unaowezesha kuweka msingi wa biashara kama kununua mashine ama vifaa…

Read More