
‘No Reforms, No Election’ yamwondoa Mwita sekretarieti ya Chadema
Dar es Salaam. Katibu wa Sekretarieti ya Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Julius Mwita ameondolewa katika wadhifa huo kwa madai kwamba amekwenda kinyume na msimamo wa chama hicho kuhusu ajenda ya “No Reforms, No Election”. Inadaiwa Mwita hakubaliani na msimamo huo na amekuwa akihamasisha wengine kupinga ajenda hiyo ambayo inalenga kuishinikiza…