
Kifo katibu wa UWT Mbeya, wabunge wamlilia wakieleza ni pigo kuelekea uchaguzi mkuu
Mbeya. Wakati mwili wa aliyekuwa Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT), Mkoa wa Mbeya, Lucia Sule (33), ukiagwa katika kiwanja cha Soko la Uhindini, wabunge waeleza kupata pigo kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025. Mwili wa Lucia umeagwa leo jijini hapa na umesafirishwa kwa mazishi yatakayofanyika nyumbani kwao Babati, Mkoa wa Manyara….