
Vituo 10 vya bunifu kujengwa kwa gharama ya Sh15 bilioni
Unguja. Katika kukuza na kuwaendeleza wabunifu wa kidijitali na wajasirimali, vinajengwa vituo 10 vya bunifu nchini vitakavyogharimu Sh15 bilioni. Kati ya hivyo, vinane vitakuwa ni vya kukuza ujasiriamali wa kutengeneza mifumo na viwili vitakuwa vinatumika kutengeneza vifaa. Vituo hivyo vinavyojengwa katika mikoa minane, mifumo yake itaunganishwa ili fursa zinazopatikana nchini, Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)…