TIJA KWA NCHI NDIYO KIPAUMBELE CHA UTEKELEZAJI WA MRADI WA KUCHAKATA NA KUSINDIKA GESI ASILIA (LNG)- DKT.BITEKO

***********  Asema kiu ya Serikali ni kuona mradi unatekelezwa ila maslahi ya Taifa ndiyo kipaumbele  Alieleza Bunge hatua zinazochukuliwa na Serikali kuhamasisha ujenzi wa vituo vya gesi (CNG) na matumizi  Aeleza kuhusu kuundwa kwa Timu kuangalia unafuu wa gharama za umeme kwa Wananchi  Kapinga azungumzia kazi za kupeleka umeme wa Gridi Rukwa, Kagera, Katavi, Lindi…

Read More

NMB Yatambuliwa kwa Ubora Tuzo za OSHA 2025

Na Mwandishi Wetu. Benki ya NMB imetunukiwa tuzo tano muhimu kutoka Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) katika Maadhimisho ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi kwa mwaka 2025, hatua inayodhihirisha juhudi za benki hiyo katika kuhakikisha mazingira salama na yenye afya kwa wafanyakazi wake. Katika hafla hiyo iliyofanyika mkoani…

Read More

Vyombo vya habari vyatakiwa kufichua rushwa uchaguzi mkuu

Dar es Salaam. Vyombo vya habari nchini vimetakiwa kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya rushwa hususani kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Crispin Chalamila wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari katika warsha…

Read More

UVCCM yawaita vijana kujiandikisha kupiga kura, kugombea

Dar es Salaam. Katibu Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Jesca Mshama amewataka vijana kuchangamkia fursa ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kuanzia ngazi ya udiwani, ubunge katika uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 2025. Amesema Tanzania ya sasa inahitaji viongozi vijana wenye maono mapana, weledi, uadilifu na uzalendo katika…

Read More

Fyatu afyatua figa na fwakit kuhusu Kanada

Tangu nifyatukie Kanada, nimekuwa nashuhudia mambo ya ajabu toka kwa mafyatu. Wapo wanaoomba mialiko ili waje huku wagome kurejea kwao na kufanya niwatunze hadi nifyatuke. Wapo wanaonipiga mizinga tena mingine ya kijinga siyo kifyatu. Hivi, unajisikiaje fyatu ambaye ameishastaafu kukubomu dolari 500 kwa ajili ya harusi ya kitegemezi chake na si kwa ajili ya matibabu…

Read More

Lissu mahabusu, nakumbuka nyakati za madeko za 4R

Ukweli upi unapaswa kuzungumzwa? Unaompa faraja mgonjwa lakini haumsaidii kubadili hali yake? Unaomuumiza mgonjwa, ila ndiyo ukweli wenyewe? Mimi nachagua ukweli unaoweza kuonekana ukatili. Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, yupo mahabusu. Kesi inayomkabili ni uhaini. Wakati huohuo, giza limetanda kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025. Ushiriki wa Chadema kwenye uchaguzi ni majaliwa. Inategemea busara zaidi. Swali, tumefikaje…

Read More

NIKWAMBIE MAMA: Uchaguzi ni mchezo wa makosa

Kwenye mchezo wa ndondi bondia anaweza kufanya kama aliyejisahau, akakuletea uso usiokingwa na mikono yake. Mbinu hii wenyewe wanaiita “kuuza sura.” Ukiamini kuwa kajisahau, utaingia kichwa kichwa, lakini ghafla atakuwahi na kukumaliza. Mabondia wengi wameshaumizwa kwa mtindo huu, lakini mabondia wajanja hupuuza chambo hicho na kuendelea na pambano kwa kuzingatia kanuni za mchezo. Wakati mwingine…

Read More

Chondechonde tusilirejeshe Taifa kwenye enzi ya giza

Aliposhika madaraka, Rais Samia Suluhu Hassan alionyesha siyo tu nia kwa maneno, bali pia kwa matendo kwa kuchukua hatua mbalimbali zilizolenga kuliponyesha Taifa. Rais Samia alikutana na makundi mbalimbali ya kijamii, wakiwemo viongozi wa dini, kisiasa na kimila kujadiliana juu ya mustakabali wa Taifa. Alizuia ukusanyaji wa kodi kimabavu kupitia vikosi kazi, kesi za kisiasa…

Read More