Tuzo za umahiri sasa kutolewa Zanzibar
Unguja. Kwa mara ya kwanza Zanzibar imeandaa tuzo za umahiri katika mawasiliano ambazo zitashirikisha waandishi wa habari kutoka ndani na nje ya nchi. Tuzo hizo ambazo zimeandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar, Taasisi ya Uhusiano ya Umma Tanzania (IPRT) na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar, zinatarajiwa kutolewa Julai 5 mwaka huu kisiwani humu….