Debora upepo umebadilika ghafla | Mwanaspoti

KATI ya sajili zilizobamba msimu huu kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Bara katika kikosi cha Simba, basi ilikuwa ni ule wa kiungao Debora Fernandes Mavambo aliyetua akitokea Mutondo Stars ya Zambia kwa mkataba wa miaka mitatu kutokana na mashabiki kuwa na matumaini makubwa naye.

Nyota huyo mzaliwa wa Jiji la Luanda, Angola aliwakosha mashabiki wa Simba kutokana na uwezo wake wa kucheza nafasi mbalimbali za kiungo, ikiwamo namba 6 na 8 na ule moto alioanza nao siku ya Simba Day alipofunga bao moja kwa shuti kali la mbali na kuwakuna Wanasimba.

Hata hivyo, licha ya kuonyesha kiwango kizuri katika michezo michache aliyoicheza mwanzoni mwa msimu, Debora alionekana kupoteza nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha Simba.

Hii ilitokana na ushindani mkubwa katika eneo la kiungo na

Related Posts