
May 3, 2025


MNUFAIKA UKIHITIMU MASOMO, LIPA MKOPO WAKO KWA WAKATI
:::::::::: Na Dk. Reubeni Lumbagala SERIKALI kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inawajibika kupokea maombi ya mikopo na kutoa mikopo kwa waombaji waliokidhi vigezo vilivyowekwa. Bodi ya Mikopo ambayo sasa imetimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2004, hadi Februari 2025, HESLB inajivunia kutoa takribani shilingi trilioni 8.2 kwa waombaji…

KAMPUNI 2476 ZA WAZAWA ZASAJILIWA KUTOA HUDUMA MIRADI YA MAFUTA NA GESI ASILIA
:::::::::::: Kufikia Aprili 2025, jumla ya kampuni za wazawa 2,476 na wataalam wazawa 431 wamejisajili katika mfumo huo ambapo Kampuni 300 zimepata fursa za kuuza bidhaa na kutoa huduma mbalimbali kwenye miradi ya mafuta na gesi asilia. Serikali imeendelea kuimarisha ushiriki wa Watanzania katika sekta ndogo ya mafuta na gesi asilia ambapo kupitia EWURA imeendelea…

Serikali yamalizia mchakato kuifanya NEMC kuwa mamlaka
Dar es Salaam. Serikali imesema inaendelea na mchakato wa kufanya mabadiliko ya kisheria ili kulibadilisha Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuwa mamlaka kamili itakayokuwa na nguvu zaidi katika kushughulikia changamoto mbalimbali za mazingira nchini Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi, Mei 3, 2025 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa…

TaCRI yapata aina tatu mpya za Arabika zitakazokabiliana na ukame
Moshi. Taasisi ya utafiti wa Kahawa nchini (TaCRI) imegundua aina mpya tatu za kahawa aina ya Arabika yenye uwezo wa kuvumilia hali ya ukame, ikiwa ni moja ya mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuongeza uzalishaji wa zao hilo. Hayo yamebainishwa leo, Mei 3, 2025 na Mtafiti mwandamizi wa afya ya udongo katika…

Wabunge: Kilimo ikolojia suluhisho kwa mabadiliko ya tabianchi
Dodoma. Wadau wa sekta ya kilimo nchini, wakiwemo wabunge, wakulima na taasisi zisizo za kiserikali, wametoa wito kwa Serikali kuongeza uwekezaji katika kilimo ikolojia, wakisisitiza kuwa mfumo huu ni suluhisho la kudumu katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kuhakikisha usalama wa chakula kwa taifa. Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi Mei 3, 2025…

Hapi aishauri TK Movements kuanza uzalishaji
Dodoma. Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Ally Hapi, amewashauri Mtandao wa Vijana wa Taifa Letu Kesho Yetu (TK Movements) kuungana na kuchangishana ili kuanzisha miradi itakayowawezesha kupata kipato na kukuza uchumi wao. Mtandao huo ulizinduliwa Mei 25, 2024 na Naibu Spika wa Bunge, Musa Zungu, ambaye aliwasihi vijana kujiandikisha katika daftari la…

RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KULETA SERIKALI KWA WANANCHI ILI KULETA MAENDELEO – MHE. MCHENGERWA
Na John Mapepele Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imedhamiria kwa dhati kuisogeza Serikali karibu zaidi na wananchi wake hasa wale walio na kipato cha chini katika maeneo ya vijijini na…

RPC Mbeya aonya uvunjifu wa amani kuelekea uchaguzi mkuu, awapa neno vijana
Mbeya. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limewataka vijana kutumia michezo kama sehemu ya kuhamasisha amani na utulivu katika kuelekea uchaguzi Mkuu Oktoba 2025, huku likionya wavunjifu wa amani. Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Benjamin Kuzaga amesema leo Jumamosi Mei 3, 2025, katika viwanja vya Kumbukumbu ya Sokoine baada ya kushiriki mbio za pole ikiwa…

RWEBANGIRA AWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA ZAO KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe.Magdalena K.Rwebangira ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Mbeya kujitokea na kufika kwenye vituo vya kujiandikisha ili kuboresha taarifa zao kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Pamoja na kuhakiki taarifa zao kwenye Daftari la Awali la Wapiga Kura ambalo limebandikwa katika kila kituo. Mhe. Rwebangira…