Sababu tatu zilizoiangusha Yanga CAS

MABOSI wa Yanga inaelezwa jana waliitana na kujifungia ili kujadili hukumu ya kesi waliyoifungua Mahakama wa Kimataifa ya Usuluhishi ya Michezo (CAS), iliyotupiliwa mbali, huku zikitajwa sababu tatu zilizosababisha kesi kufutwa na ushauri waliopewa mabosi hao wa Jangwani.

Yanga ilikimbilia CAS baada ya mechi ya Dabi ya Kariakoo dhidi ya Simba kuahirishwa saa chache kabla ya kufanyika Machi 8, mwaka huu, ikidai kanuni za ligi zilikiukwa kimakusudi ili kuinufaisha Simba iliyotangaza isingecheza kwa kuzuiwa kufanya mazoezi ya mwisho Kwa Mkapa na mabaunsa wanaodaiwa kuwa wa Yanga. Hata hivyo, juzi hukumu ya kesi hiyo ilisambaa mtandaoni ikielezwa imefutwa na Bodi ya Ligi kutoa taarifa kuwa ilikuwa ikijianda kutoa ratiba mpya ya pambano hilo na mengine yaliyobaki ya ligi iliyosaliwa na raundi tatu kabla ya kufikia tamati. Mapema jana asubuhi ilielezwa mabosi wa Yanga waliitana ili kujadili na walikuwa wakijiandaa kutoa taarifa  ya klabu, lakini mwanasheria na mwandishi mzoefu wa habari za michezo, Wakili Alloyce Komba aliyewahi kuwa wakili wa Yanga enzi za Yusuf  Manji ametaja sababu tatu za kesi hiyo kufutwa na kwamba kila kitu kimeshaisha na Yanga iendelee na mambo mengine tu kwa sasa.

Akizungumza na Mwanaspoti, Komba alisema kesi ya Yanga haipo kwa sababu kuu tatu ambazo alizitaja kuwa ni CAS imekosa mamlaka ya kusimamia kesi hiyo, kukosa hukumu iliyoifanya Yanga kukimbilia CAS na kushindwa kukamilisha mchakato kwa kufuata utaratibu.

“Kuna ngazi zimerukwa, hivyo CAS wamegundua kanuni ya TFF Ibara ya 26.26 au ukianzia 22 kuna kamati ya rufaa na Yanga haikuanzia huko kwa kufuata mchakato na badala yake wamekwenda moja kwa moja kule,” alisema Komba na kuongeza: “Hakukuwa na uamuzi ambao umetolewa na Bodi ya Ligi na TFF ambao uliifanya Yanga wakate rufaa hukumu waliyokuwa nayo ni kuahirishwa kwa mchezo ambayo imekataliwa na CAS, lakini pia walikuwa na malalamiko ya matumizi ya fedha huku wakiwa hawana viambatanisho.”

Alisema kwa mantiki hiyo Yanga haina kesi ya kusikilizwa na kuhusu kurudi haoni kama kutakuwa na nafasi kwa sababu kuna ukomo wa kusikiliza kesi za aina hiyo kwa kujaribu kurudi kufuata utaratibu.

Komba alisema Yanga inachotakiwa kufanya ni kufuata utaratibu itakaopewa na Bodi ya Ligi hasa kwenye mchakato wa kupokea maelekezo na kutekeleza. “Lakini, Yanga inatakiwa kulinda heshima na rais wa klabu hiyo, Hersi Said ambaye ni kiongozi mkubwa wa CAF wanamuweka kwenye hatari.”

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa zamani wa TFF, Angetile Osiah, alisema kilichotokea kwa Yanga ni kutokana na Kamati ya Kusimamia na Kuendesha Mashindano ya Lihi kupewa mamlaka makubwa ya kutoweza kupingwa baada ya kufanya uamuzi wowote.

“Wakati tunaanzisha hii kamati ilikuwa imelenga kupitia na kusimamia kile kinachoripotiwa na waamuzi ndani ya dakika 90 za mechi, lakini imebadilishwa na kupewa majukumu makubwa yasiyopingwa na hivyo, Yanga iliamua kukimbilia CAS,” alisema Angetile.

“Kwa kawaida maamuzi yanayofanywa na chombo cha juu, haiwezekani tena kuanzishwa mchakato mpya juu ya kesi husika. Najua Yanga imejifungua kujadili hukumu, lakini kwa ushauri wangu ingeachana nayo na kukubali kucheza dabi, kwani timu yoyote ina nafasi ya kushinda.

“Ninachojua Yanga imefanya ilichokifanya kutaka kukumbusha mamlaka juu ya umuhimu wa kuzingatia kanuni na kuzitekeleza bila upendeleo au kuegemea kwa baadhi ya klabu.

“Ukifuatilia Simba ilitoa tishio la kutocheza na kusema ising-echeza ligi hadi waliohusika kuwazuia kufanya mazoezi waadhibiwe. Cha ajabu hadi leo waliohusika hawajaadhibiwa na Simba imecheza mechi za ligi ikiwamo ya jana. Hii ni kuonyesha haikuitaka dabi na Bodi iliingia kwenye mfumo wao.”

Angetile alisema anadhani baada ya msimu kumalizika Yanga ihamasishe klabu nyingine kuibana Bodi ya Ligi kusimamia kanuni inazoziweka na kwa vile rais wa Yanga, Injinia Hersi Said ni mwenyekiti wa klabu za soka Afrika, anaweza kujifunza kupitia ligi zingine kuona jambo hilo halijirudiii tena.

“Kwa msingi huo ni kwamba mashabiki kwa sasa wanasikilizia juu ya ratiba mpya ya Dabi ya Kariakoo ambayo Yanga ilitishia kuicheza kwa madai ilistahili kupewa ushind

Related Posts