
May 4, 2025


VIBALI SITA VYATOLEWA USAMBAZAJI GESI ASILIA VIWANDANI, TAASISI
::::::::::::: Hadi Aprili, 2025 EWURA ilitoa vibali sita (6) vya ujenzi wa mabomba ya kupeleka gesi asilia kwenye viwanda, taasisi, migahawa ya chakula na majumbani. Kati ya vibali hivyo, kibali kimoja (1) kilitolewa kwa Kampuni ya PAET kwa ajili ya ujenzi wa bomba la kupeleka gesi asilia kwenye kiwanda cha Aluminium Africa (ALAF) Jijini Dar…

TANZANIA KUMILIKI TEKNOLOJIA YA VIUATILIFU HAI KUTOKA CUBA
::::::::: TANZANIA na Cuba zimesaini mkataba wa kuhamisha teknolojia ya utengenzaji wa Viuatilifu Hai (Biolarvicides) kwa ajili ya kutokomeza ugonjwa wa malaria na wadudu waharibifu wa mazao ya kilimo. Mkataba huo umesainiwa baina ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), kupitia Kampuni tanzu ya Tanzania Biotech Products Limited (TBPL)…

MFAHAMU TORONTO; KIJANA ANAYEANDIKA HISTORIA YA MAENDELEO KUPITIA CCM SONGEA
*Ni msomi wa elimu ya juu aliyoipata Canada na sasa ameamua kupiga Kambi Ruvuma *Mkakati wake ni kuchangia maendeleo ya Jamii, kukuza thamani ya CCM Na Belinda Joseph-Songea. KATIKA kizazi cha sasa kinachotawaliwa na ndoto nyingi lakini vitendo vichache, jina la Amandius Jordan Tembo maarufu kama Toronto, linaibuka kama nembo ya matumaini mapya ya maendeleo…

BARABARA KOROFI YA MABOGINI – KAHE KUJENGWA KWA LAMI- MHE MCHENGERWA
Na John Mapepele -Moshi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa leo amekagua uharibifu wa barabara ya Spencon- Fongagate- Mabogini- Chekereni hadi Kahe yenye urefu wa kilomita 31.25 na kuiagiza Wakala ya Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) kuanza mara moja kujenga kwa kiwango cha lami. Akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi…

Rais Ruto apigwa na kiatu akihutubia, watatu watiwa mbaroni
Migori. Katika hali isiyo ya kawaida, Rais wa Kenya, William Ruto, amejikuta akipigwa na kiatu mkononi kilichorushwa kutoka kwenye umati wa watu aliokuwa akiwahutubia katika mji wa Kehancha Magharibi mwa Kenya. Tovuti ya Nation ya nchini humo imeripoti kuwa tukio hilo la kushtukiza kwa Ruto limetokea leo Jumapili, Mei 4, 2025, katika siku ya tatu…

Moto, uvamizi watishia urithi wa dunia nchini
Serengeti. Majanga ya moto na uvamizi wa watu katika maeneo ya hifadhi za Taifa yameendelea kuwa tishio kwa maeneo ya urithi wa dunia na vituo vya urithi wa Taifa hapa nchini. Wataalamu wanataka hatua za haraka kuchukuliwa ili kuyalinda maeneo hayo dhidi ya uharibifu wa kudumu. Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Stephano Msumi…

Polisi kuchunguza tuhuma askari kuhusishwa kupotea kwa mdude
Dar es Salaam. Jeshi la Polisi limetangaza kuchunguza tuhuma za kuhusika kwa askari katika tukio la kupotea kwa mwanaharakati na kada wa Chadema, Mdude Nyagali huko mkoani Mbeya. Taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii usiku wa kuamkia Mei 2, 2025 saa 8:00 Mdude akiwa amelala nyumbani kwake Mtaa wa Ivanga, Kata ya Iwambi, jijini Mbeya,…

TEC: Shambulio la Padri Kitima linagusa maeneo matatu
Dar es Salaam. Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limesema shambulio dhidi ya Katibu wa Baraza hilo, Padri Charles Kitima, licha ya kumuumiza yeye, pia baraza hilo limeshambuliwa na heshima ya Taifa imejeruhiwa. Kauli hiyo imetolewa katika salamu za TEC zilizotolewa na Makamu wa Rais wa Baraza hilo, Askofu Eusebius Nzigilwa leo Jumapili Mei 4,…

KIDATO CHA SITA KUANZA MITIHANI KESHO, MAANDALIZI YAMEKAMILIKA
:::::::::: HABARI Baraza la Mitihani Tanzania NECTA limetangaza kuanza kwa mitihani ya kidato cha Sita na Ualimu inayotarajiwa kuanza Kesho Jumatatu Mei 5.2025 nchi nzima Akizungumza na wanahabari Jijini Dar es salaam Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini (NECTA) Dkt. Said Mohammed amesema jumla ya watahiniwa 134,390 wamesajiliwa kufanya…