Fadlu ashtukia mchongo, apanga upya silaha zake

KOCHA Mkuu wa Simba, Fadlu Davis amesema anafanya mabadiliko ya kikosi chake kutokana na ugumu wa ratiba na ataendelea kufanya hivyo kwa kuwapa mapumziko ya kutosha nyota wake ili kufikia malengo.

Kwa sasa Simba inacheza mechi za viporo za Ligi Kuu Bara kabla ya kwenda kucheza mechi ya fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane.

Akizungumza na Mwanaspoti, Fadlu amesema ratiba upande wao ni ngumu lakini anawapongeza wachezaji wake kwa kufuata maelekezo anayowapa na kuipambania timu kupata matokeo mazuri huku akiamini wataendelea kufanya hivyo na kufikia malengo ya kutwaa mataji.

“Kucheza mechi nne ndani ya siku kumi sio jambo rahisi, tuna siku mbili katikati ya mechi ya Pamba na KMC, sio rahisi kuingia na kikosi kilekile, nitafanya mabadiliko bila kufuata mfumo lakini naamimi tutapata matokeo mazuri,” amesema na kuongeza.

“Jumanne tutafanya tathmini, tutapokea ripoti ya madaktari na kufanya ‘recovery’ ili tupate kikosi cha kuikabili Pamba, sio rahisi lakini nina imani kubwa na wachezaji wangu

Related Posts