Dar es Salaam. Muasisi wa Kituo cha Maombezi cha Mama Bikira Maria (Marian Faith Healing), Padri Felician Nkwera (89) amefariki dunia.
Waamini wamekusanyika katika kituo hicho kilichopo Ubungo Riverside, Dar es Salaam leo Mei 9, 2025 kuomboleza.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kituoni hapo, Padri Nkwera alifariki dunia jana Alhamisi Mei 8, 2025 usiku.
“Aliaanza kujisikia vibaya jana asubuhi akiwa kanisani, hivyo aliporejeshwa nyumbani kwake, madaktari walipompima walibaini presha yake ipo chini, lakini muda wa jioni hali ilibadilika wakampeleka Hospitali. Hata hivyo ikaonekana presha yake ilikuwa sawa na akaruhusiwa kurudi nyumbani, lakini wakiwa njiani hali yake ikabadilika kisha wakampeleka Hospitali ya TMJ, huko ndipo alifikwa na umauti,” kilieleza chanzo cha taarifa.
Padri Nkwera aliwahi kuhudumu Kanisa Katoliki kabla ya kutengwa na uongozi wa kanisa hilo.
Endelea kutufuatilia Mwananchi.