:::::
Serikali imedhamiria kununua mtambo maalum wa kusafisha ziwa victoria lililoathirika na gugumaji jipya ambalo limekuwa tishio kwa shughuli za uvuvi na usafirishaji kwa wananchi.
Hayo yamesemwa Jana Mei 10, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda alipokua akizungumza na Wananchi waliokuwa wakisubiri huduma ya usafiri wa kivuko katika eneo la Kigongo Wilayani Misungwi mkoani Mwanza
Amesema mpaka sasa fedha tayari zimeshatengwa na taratibu za manunuzi zimeshaanza na muda si mrefu mtambo huo utawasili na kazi hiyo ya uvunaji wa magugu maji itaanza .