MKOA wa Iringa umeanza mkakati wa kujenga uwanja wa kisasa wa gofu utakaojulikana kama Mkwawa Golf Course ili kuendeleza mchezo huo mkoani huo na nchini kwa jumla.
Kwa miaka mingi Iringa imekuwa na uwanja mmoja wa gofu wa Mufindi uliojengwa na Kampuni ya kikoloni ya Brooke Bond uliopo katika mashamba ya chai na wazo hilo lilitolewa na wachezaji wakongwe wa mchezo huo kutoka mkoa huo, Edmund Mkwawa na Alfred Kinswaga waliofika katika Klabu ya Lugalo, jijini Dar es Salaam.
Nahodha wa gofu katika klabu ya Lugalo, Meja Japhet Masai, Mweka Hazina, Kapteni Mtuya na Mratibu wa Chama cha Gofu Tanzania, Johnson John ndio walioupokea u