KAILIMA AONYA WATAKAOVURUGA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Sambamba na hayo amewataka wananchi kuacha tabia ya kuchana au kuharibu karatasi za orodha ya wapiga kura zilizobandikwa kwenye vituo vya kujiandikishia kwani kitendo hicho kinaweza kuzuia watu wengine kuhakiki taarifa zao, jambo ambalo linaweza kuwanyima haki yao ya kupiga kura iwapo taarifa zitakuwa na hitilafu.

Kwa upande wake, Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Kilosa na Mikumi, Betuely Ruhega ameishukuru Tume kwa kurahisisha mchakato wa uandikishaji, ambapo sasa mtu anaweza kujiandikisha au kubadilisha taarifa zake kwa njia ya mtandao, kisha kwenda kituoni kuchukua kitambulisho chake bila kupoteza muda jambo ambalo limetoa fursa kwa watu kuweza kujiandisha na kuahakiki taarifa zao.

Ameongeza kuwa mfumo huo ni rafiki kwa watu wote, wakiwemo wenye ulemavu, kwani waandishi wasaidizi na waendesha vifaa BVR wamepewa maelekezo ya kuzingatia hali ya kila mtu wakati wa kuchukua alama za vidole, picha na saini.

Uboreshaji wa daftari hili unalenga kuwapa nafasi wapiga kura wapya kujiandikisha, pamoja na kuwahakikishia wapiga kura waliopo kuwa taarifa zao ni sahihi kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Pili litaingia katika mzunguko wa pili kuanzia Mei 16 hadi Mei 22, 2025, likihusisha mikoa ya Pwani, Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Dodoma, Singida, Manyara, Lindi, Mtwara, Morogoro na Dar es Salaam kwa upande wa Tanzania Bara pamoja na Mikoa yote ya Tanzania Zanzibar.

Mkurugenzi wa Tume Huru ya Uchaguzi, Ramadhani Kailima, akizungumza katika mafunzo ya waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya Bayometriki (BVR) wa Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro, Mei 15, 2025 ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya awamu ya pili ya mzunguko wa pili wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, litakalofanyika kuanzia Mei 16 hadi 22, 2025. Picha na INEC.

Mkurugenzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ramadhani Kailima, akizungumza katika mafunzo ya waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya Bayometriki (BVR) wa Wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro, Mei 15, 2025 ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya awamu ya pili ya mzunguko wa pili wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, litakalofanyika kuanzia Mei 16 hadi 22, 2025. Picha na INEC.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura (Elimu), Dkt. Rose Likangaga akitoa elimu ya Mpiga Kura katika mafunzo ya waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya Bayometriki (BVR), Wilayani Mvomero, Mkoa wa Morogoro, Mei 15, 2025, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya awamu ya pili ya mzunguko wa pili wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, litakalofanyika kuanzia Mei 16 hadi 22, 2025. Picha na INEC.