Wadau waitwa kusaidia utunzaji mazingira, elimu

Dar es Salaam. Katika kuendeleza ubora wa elimu pamoja na mazingira salama na wezeshi kwa wanafunzi wadau wa maendeleo wameombwa kujitolea vifaa saidizi ikiwemo taulo za kike, pipa za kuhifadhia uchafu katika shule mbalimbali nchini.

Wito huo umetolewa na wazazi pamoja na walimu leo Mei 26, 2025 wakati wakipokea msaada wa vifaa mbalimbali vya kuwezesha ufundishaji kutoka taasisi ya GSM Foundation katika shule ya msingi Mtoni Kijichi iliyopo Temeke Dar es Salaam.

Katika msaada huo vimetolewa viti mwendo vinne kwa wanafunzi wenye ulemavu, vifaa vya kusaidia usikivu (Assistive listening devices (ALDs) kwa wanafunzi kumi wenye usikivu hafifu na maboksi kumi ya nepi kwa ajiri ya kusaidia wanafunzi ambao hawawezi kuthibiti hali zao wawapo darasani.

GSM Foundation pia imetoa elimu juu ya hedhi salama kwa wanafunzi 500 ambao ni balehe katika shule iyo na kukabidhi jumla ya boksi 100 ya taulo za kike ili kuwawezesha wanafunzi wa kike kufurahia wawapo katika kpindi cha hedhi.

Akizungumza baada ya kupokea kitimwendo kwa mtoto wake mwenye uhitaji maalumu mzazi Halima Salehe amesema mwanaye aliyepata kitimwendo kitamsaidia kumleta shule na kumrudisha nyumbani.

“Nilikuwa napata shida kumleta mwanangu shuleni, wakati mwingine amekuwa akichelewa vipindi lakini sasa kupitia kitimwendo anakuja shule vizuri,” amesema.

Mwanafunzi wa shule hiyo Careen Mtui anayesoma darasa la nne amesema pia, wangepewa na vitabu viongezeke maktaba ili kuongeza ufaulu zaidi.

“Tunaomba na kila mwanafunzi apate vitabu pia vya kujifunzia kwaajili ya kuongeza ufaulu zaidi,” amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Butiama ilipo shule hiyo, Mohamed Hegga amesema watoto wenye uhitaji maalumu wanawapa changamoto wazazi wao kuwahudumia hivyo msaada wakiopata utawasaidia kwa kiasi kikubwa.

Aidha taasisi hiyo imesimika mapipa 12 ya kuhifadhia taka kwa matumizi ya nje ya madarasa, vipipa taka 25 vya ndani ya madarasa, toroli moja la usafirishaji wa taka na kubandika mabango 50 yenye jumbe za kimazingira kwenye mazingira ya shule.

Akizungumza kwa niaba ya walimu, mwalimu Marry Kiviro amesema kabla ya kuletewa msaada huo walikuwa wakipata shida kukusanya uchafu na sehemu za kuuweka.

“Tunashukuru tunakusanya usafi tunaweka kwenye mapipa. Watoto wetu wenye ulemavu hawakuwa na sehemu za kuandika na sasa wamepata. Tunahitaji msaada zaidi ikiwemo vifaa vya Tehama kama kompyuta, vishikwambi ili kusaidia kujifunza zaidi,” amesema.

Akizungumza kwa niaba ya uongozi wa shule, Mkuu wa shule, Twaha Kifunde amepongeza jitihada za GSM Foundation Pamoja na GSM Group katika kuunga juhudi za serikali ili kuhakikisha utekelezaji wa elimu jumuhishi na mazingira rafiki ya kujifunzia wa wanafunzi.

Ameongeza kua kupitia upatikanaji wa vifaa vya kukusanyia na kuifadhia taka, vifaa saidizi kwa watoto wanaoishi na ulemavu na upatikanaji wa taulo za kike vitasaidia upungufu wa tatizo la utoro kwa watoto hao huku vikirahisisha kazi za walimu wakati wa ufundishaji.

Kupitia msaada wa sabuni za Ng’arisha, Mkuu amesema anategemea wanafunzi watakua wasafi na kuwahakikishia wananchi kua ili kuthibitisha ilo, watembelee shule iyo kushuhudia wenyewe.

Mkuu wa shule amesema anashukuru kwa msaada huo ambapo amesema taasisi kama hiyo kutambua changamoto za shule hususanj kitengo cha mafunzo ya wanafunzi wenye ulemavu wa akili ni jambo la kuungwa mkono.

“Kwa niaba ya ofisa elimu na Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke tunashukuru. Tunachangamoto ya madawati tunaomba mtuangalie kwa jicho lingine,” amesema Mkuu huyo.

Kwa upande wake Mkuu wa GSM Foundation, Faith Gugu           amesema mpango huo ni sehemu ya dhamira ya GSM Foundation ya kusaidia utekelezaji wa Sera ya taifa ya Mazingira ya 2021 ambayo inasisitiza ushiriki wa sekta binafsi katika uhifadhi na utuaji wa mazingira.

Pia, katika utekelezaji wa Mpango wa elimu jumuishi, GSM Foundation inaendelea kutekeleza na kuunga mkono sera za kitaifa na kimataifa ikiwepo “Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu wenye Ulemavu (2006)”.

Kabla ya utekelezaji huo, ilibainika kwamba kwa sababu ya ukosefu wa taulo za kike, ilisababisha utoro na kupunguza  maudhurio hasa katika siku ambazo binti anakaua kwenye hedhi.

Kwa mwanamke/msichana ambae Afya yake iko vizuri, anaingia hedhi siku tano hadi sita hivyo basi wakati wanapata changamoto ya taulo za kike kila mwezi binti anaweza kukosa masomo siku hizo ambapo kwa mwaka katika miezi kumi ya masomo anauwezekano wakukosa masomo siku 60 kwa  wanafunzi wa shule za msingi.

Ili kusisitiza upatikanaji wa taulo za kike shuleni amesema; “Serikali haina budi kuandaa sera ya upatikanaji wa Taulo za kike Kwa shule za msingi hadi kidato cha Sita. Kama zilivyo sela za Ukimwi upatikanaji wa kondomu bure.

“Sera za uzazi wa mpango sera ya kuzuia na kupambana na malaria bure sera za kuwasidia watu walio athirika na dawa za kulevya, vivyo hivyo upatikanaji wa taulo zakike unahitajika kwa kiwango kikubwa katika shule nyingi haswa kwa mashule yanayopatikana maeneo ya pepmbezoni na  vijijini”amesisitiza

Related Posts