Dar es Salaam. Aliyekuwa kada wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) na mmoja wa waasisi wake, Eugen Kabendera amedai ujio wa waliokuwa makada wa Chadema kwenye chama hicho, unakwenda kumeza sera za kuanzishwa kwake.
Jumanne Mei 27, 2025 Kabendera aliye-dumu kwa miaka 13 katika chama hicho, alitangaza kuondoka ndani Chaumma kuto-kana na tofauti ya mtazamano na mwele-keo wa sasa wa Chaumma baada ujio wa makada wapya kutokea Chadema.
Mwananchi limefanya mahojiano maalumu na Kabendera alipotembelea ofisi za Mwananchi Communications Limited (MCL), hivi karibuni, ambapo ame-zungumzia masuala tofauti na kilichomwondoa Chaumma.
“Nikuambie wengi wape, kulingana na wingi wao watashinikiza kutekelezwa mi-pango yao na kusahau misingi thabiti ya kuanzishwa kwa Chaumma ninayoijua. Sitaki kuwa mpinzani ndani ya chama changu, nimeona niondoke niwaachie wao,” anasema Kabendera.

Wakati Kabendera akitoa madai hayo, Nai-bu Katibu Mkuu mpya wa Chaumma (Bara), Benson Kigaila amemjibu kuwa ujio wa G55 ndani ya chama hicho, hauwezi kumeza se-ra zake, wala kupeleka sera za jukwa walilo-toka.
“Tukuja Chaumma hatuwezi kuja na sera za Chadema, tutatumia sera zao kwa sababu zipo kwenye katiba. Lakini sera za Chaum-ma zitafafanuliwa zaidi,” amesema Kigaila
Katika maelezo yake, Kabendera amesema kundi lililoingia Chaumma ni kubwa na limekwenda kukimeza huku wageni waki-tunukiwa nyadhifa za juu ndani ya chama hicho.
“Tafsiri yake watakuwa na ushawishi mkubwa wa kutengeneza mipango yao na kutaka itekelezwe, naenda kutafuta jukwaa la watu wenye malengo yanayofanana na dhumuni kubwa ni kushika dola.
“Kama Chaumma wanaona uelekeo wa sasa watashika dola basi waendelee lakini kwangu sioni kama kuna mwanga mbele,” amedai.
Taarifa za G55 kutua Chaumma
Kwa mujibu wa Kabendera, ujio wao maka-da wapya ndani ya chama hicho, hakushiri-kishwa licha ya kuwa mmoja wa waasisi, badala yake alisikia uvumi kupitia mitandao ya kijamii.

“Kuwa kwangu kada wa kawaida ndani ya chama ndiyo sababu ya kutokushirikishwa, badala yake nimekuja kuona wanaanza kupokelewa rasmi Mei, 19, 2025.
“Nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu tangu kupokelewa kwao wamekuwa waki-zungumzia zaidi nafasi za ubunge kuliko matatizo ya wananchi, nikagundua itikadi zao pamoja na falsafa zao haziendani na misingi ya Chaumma niliyoshiriki kuiasisi,” anasema Kabendera.
Kuhusu madai ya kutoshirikishwa kwenye mchakato wa kuwapokea makada walioto-ka Chadema, Mwenyekiti wa Chaumma, Hashim Rungwe amemjibu Kabendera akisema kwa kifupi kwamba kila jambo lina wakati wake.
“Kabla ya kufikia uamuzi wa kuwapokea mamia ya makada kutoka Chadema nili-washirikisha viongozi wenzangu lakini Kabendera hakujulishwa.
“Nilipopata taarifa ya awali kuhusu ujio wao, nilizungumza na viongozi wenzangu, wakakubali na kuachia nafasi walizozihitaji makada wapya,” amesema.
Rungwe ameongeza kuwa: “Kabendera ka-ma muasisi sikumjulisha kwa sababu haku-wa mwanachama hai tangu Septemba 2024 aliposusa baada ya kuteuliwa kuwa Msema-ji wa Chama tangu hapo alikaa kimya, hakujishughulishi na chama,” amesema.
Hata hivyo, Kabendera anasema wanacha-ma hao wapya wanaamini kwenye ubunge badala ya kujikita kulitumia jukwaa hilo, kuzungumza shida za wananchi na mikakati watakayoitumi kuzitatua.
“Wananchi wanakabiliwa na changamoto ya mikopo ya kausha damu, ajira kwa vijana zilikuwa ajenda za msingi kwa nyakati hizi kujitokeza kwa wananchi na kuja mawazo mbadala ya kuwakwamua ili kuandana na dhana ya chama cha Ukombozi wa Umma,” anasema.

Kabendera anasema wanahitaji ubunge wanashindwa kutambua hilo ni suala la uwakilishi wa watu na ni wachache wana-weza kupata fursa hiyo, lakini si kusema kila mmoja anataka kwenda bungeni ni jambo ambalo haliwezekani.
“Kuna mambo mengi mazito ambayo jamii inahitaji kusemewa na kuhakikisha mabadil-iko yanapatikana nilikuwa nategemea hivyo na ndicho naamini na si kugombea, maba-diliko ya kweli ni kubadilisha maisha ya Wa-tanzania waondokane na umaskini unaowakabili,”anasema.
Aikumbuka sera ya ‘ubwabwa’
Kabendera anasema hata wakati wanafikir-ia kuja na sera ya ‘ubwabwa 2015’ shuleni na hospitali, chakula kitolewe bure, walikuwa wanajua ajenda hiyo inawahusu watu wengi wanaoshinda njaa.

“Shuleni watoto wanashindishwa njaa mtu mwenye njaa hawezi kujifunza na kupata maarifa na ujuzi unaohitajika, na mtu akiwa hospitali wapatiwe chakula na gharama hizo ibebe serikali tumezungumza mara nyingi,” anasema.
Anasema baada ya kuona chama hicho ki-mechukua mkondo huo asiwe kizingiti kwenye taasisi hiyo na anatafakari kwa kina kuona ni jukwaa gani sahihi anaweza akatimukia kwenda kufanya siasa za kupi-gania kuwa komboa wananchi.
“Nitaenda kwenye chama kinachoendana na mitazamo, msimamo itikadi na sera am-bazo naamini zinaenda kuwatetea wanan-chi na Tanzania ina vyama 19 vya siasa ni haki ya kila mtu kuchagua ajiunge na chama gani,” anasema.
Kabendera anasema nafsi yake inamsuta badala ya kupinga sera ndani ya chama hicho anachodai kimekengeuka malengo ya kuanzishwa kwake ameona atupe taulo mapema.
Kabendera anasema kukaa kwake kimya kunatumika kama turufu ya kutaka kupuuza hoja anazozieleza ambazo ziko wazi ingawa mara ya mwisho kuhudhuria mkutano wa kamati kuu ya chama hicho ilikuwa mwishoni mwa Februari 2025.

Aliyekuwa kada wa Chaumma, Eugene Kabendera akizungumza na mwandishi wa Mwananchi wakati wa mahojiano maalumu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Picha na Sunday George.
“Ukimya wangu uko wapi na huu na hii ni Mei na Kamati Kuu nilihudhuria Februari 2025 huu ni ukimya gani? Wanapimaje ukimya wangu kama mikutano muhimu nilikuwa na hudhuria,” anasema.
Anasema anachojua chama cha siasa ni wanachama hadi Chaumma kinafikia uamuzi huo tafsiri yake waliowengi waliku-baliana lakini baada ya kuona jambo hilo na kulinganisha na msimamo waliokuwa nao kwa muda mrefu thamiri yake inamtuma ni wakati wa kuondoka.
Kabendera anasema anayojivunia kwani ni kuwa miongoni mwa waasisi wa chama hicho ambacho kwake kilimtambulisha kwenye ulingo wa kisiasa.
“Najivunia kwa hilo,nilitumia muda wangu mwingi katika kukitumikia chama na katika nyakati ngumu likuwa kipindi cha chaguzi kusimamisha mgombea urais si jambo jepesi,”anasema.
Anasema pamoja na ugumu huo lakini walipambana na walifanikiwa kuweka mgombea kwa kushirikiana na wenzake kwa upande wa Tanzania na Zanzibar kika-milifu.
“Tulishiriki nafasi za ubunge tulipata tuli-chopata baada ya kuaminiwa na wananchi tulishika nafasi ya sita kati ya vyama 19 vya siasa,”anasema Kabendera.

Naibu katibu mkuu bara wa chauma, Rahman Rungwe akitangaza kujiuzulu nafasi hiyo mbele ya Halmashauri Kuu ya chama hicho.
Anasema walikiendesha chama hicho kwa miaka yote hiyo kikiwa hakipati ruzuku yalikuwa maisha magumu lakini walivumilia ingawa kuna wakati walikuwa wana-shirikiana na Watanzania wenye nia njema.
“Tulikuwa tunapata mahusiano mazuri na vyombo vya habari ikiwemo Mwananchi Communication Limited,” amesema.
Anasema Rungwe na yeye kilichowafanya kuwa karibu ni siasa na wafikishana hadi walipofikia akiwa kiongozi na amemfun-disha mengi ya kiuongozi na maisha kwa ujumla.
“Nimekuwa karibu naye kisiasa, tumetofau-tiana kwa sasa tu lakini bado ataendelea kuwa mzazi wangu siwezi kusema uongo kanifundisha mengi nje ya siasa na siwezi hata kuyataja,” anasema.

Anasema nje ya hilo lililotokea, Rungwe ni mmoja kati ya watu wanapambanaji wazuri na ni mfanyabishara mkubwa na amemfun-disha katika mapambano asikubali kukata tamaa mapema.
“Ni mtu ambaye amekuwa sehemu kubwa ya makuzi yangu katika medani za siasa,”anasema
Kuhusu hatma yake kisiasa, Kabendera anasema yeye bado ni kijana mbichi hawezi kuacha siasa, ataendelea kuzifanya kwaku-wa dhamira yake ya kuwapigania watanza-nia katika kupata mageuzi ya kweli bado haijatimia.
“Ingawa kikubwa kwa sasa naangalia ni chama gani na weza kwenda kuingia kinachoendana na maono yangu na wanaosimamia kile wanachokiamini, hawa Chaumma wao waendelee,” anasema.
Kigaila, katika mahojiano yake na Mwanan-chi, alisema wamekwenda Chaumma kwa makubaliano na viongozi na ujio wao utakwenda kukikuza chama hicho katika ulingo wa kisiasa.
“Kundi letu ni kubwa sawa lakini kama wao waliweza kuwa na chama kwa muda mrefu wakashindwa kulifanya kundi lao kuwa kubwa leo wakipata kundi kubwa wana-chukia. Kundi kubwa linakukuza chama,” alisema Kigaila.