Shinyanga. Shirika la Madini la Taifa (Stamico) linatarajia kuwapatia vifaa vya kisasa vya uchakataji wa madini wanawake hao kupitia Chama cha Wanawake Wachimbaji Tanzania (Tawoma)
Lengo la msaada huo ni kuhakikisha wanawake waliopo katika sekta ya madini wana-shiriki kikamilifu kwenye uvunaji wa rasili-mali hizo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Stamico, Dk Venance Mwasse amesema hayo Mei 29, 2025 wilayani Kahama mkoani Shinyanga, wakati akizungumza na wanawake wachimbaji kutoka mikoa ya kimadini ya Kahama, Shinyanga na Simiyu.
Ahadi hiyo ya Stamico imetokana na ombi la Mwenyekiti wa Tawoma Taifa, Semeni Malale, kuwa wanawake wachimbaji wawezeshwe kwa nyenzo za kisasa ili washiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji mali kupitia sekta ya madini.
Vifaa hivyo, ambavyo ni mashine za kupon-da mawe yanayodhaniwa kuwa na dhahabu (Joo Karasha) na drone 10 zenye vifaa vya kufanya tafiti za kina kwenye maeneo ya madini, vinatarajiwa kukabidhiwa Juni 2025 katika ofisi za Stamico jijini Dodoma.
Dk Mwasse amesema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha wananchi wanavuna rasilimali za madini na kuwawezesha wachimbaji wadogo au wazawa kupitia Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Tanzania (Femata), wakiwemo Tawoma, ili waweze kuchimba kwa tija.
“Hiyo ni dhamira ya dhati ya Serikali ya ku-wawezesha Watanzania kushiriki kwenye uvunaji wa rasilimali za madini, hasa wali-opo kwenye muhimili wa Femata, ikiwemo Tawoma,” amesema.
Kwa mujibu wa takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya 2022, kati ya ajira milioni 6 zinazotokana na wachimbaji wazawa wa madini, Tawoma imeshikilia ajira milioni 3.1, sawa na asilimia 52. Kwenye takwimu hizo, ajira milioni 4.08, sawa na asilimia 67 ya wachimbaji wote Tanzania, ni vijana.
Dk Mwasse ameihimiza Tawoma kushika-mana, kuvumiliana na kutatua changamoto ndogondogo kabla hazijaota mizizi na ku-watoa kwenye malengo yao.
“Rai yangu kwenu, kwa niaba ya Tawoma Taifa, tuendelee kushikamana. Hakuna jambo jema kuliko mshikamano baina yenu wenyewe lakini pia na mzazi wenu ambaye ni Femata,” amesema.
Aidha, ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka minne, Tawoma kupitia kikundi cha Mshikamano kilichopo Kijiji cha Nyamishi-ga, wilayani Kahama, imechangia zaidi ya Sh4 bilioni kwenye mapato ya Serikali.
Kuhusu dhana potofu kwamba wanawake hawaruhusiwi migodini wanapokuwa kwenye hedhi ikidaiwa ni mikosi, Malale amesema elimu inaendelea kutolewa kuondoa imani hizo.
“Hizo ni imani potofu zilizokuwepo hapo awali, lakini sasa hali hiyo haipo tena. Tunaendelea kutoa elimu kwa wanawake na wengi wanajitokeza kuwekeza kwenye sekta hii ya madini,” amesema Malale.
Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji madini Mkoa wa Shinyanga (Shirema), Hamza Tandiko ameiomba Tawoma kutoa mafunzo endelevu yatakayowawezesha wachimbaji kufuata sheria na taratibu za uchimbaji salama, unaozingatia utunzaji wa mazingira.
Mmoja wa wachimbani wanawake, Agnes Kahabi ameeleza kuwa kutokana na uhaba wa ajira, vijana wengi wasomi na wasio wasomi wamekimbilia kwenye sekta ya madini, hivyo ni muhimu kwa Serikali kupitia Stamico kuongeza nguvu katika ku-wawezesha vifaa vya kisasa na mitaji ili wanufaike zaidi na sekta hiyo.