Dar es Salaam. Kamishna wa Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji mstaafu, Sivangil-wa Mwangesi amesema hali ya maadili nchini imekuwa ikiimarika kutokana na kuongezeka kwa uadilifu kwa viongozi wa umma.
Jaji Mwangesi amesema hilo limepimwa kwa kuangalia uzingatiaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Namba 13 ya mwaka 1995 na ujazaji wa matamko ya rasilimali na madeni kwa viongozi ambao idadi imekuwa ikiongezeka kila mwaka.
Akizungumza na wanahabari leo Mei 30, 2025 wakati wa warsha maalumu kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Jukwaa la Wahariri Tanzania, amesema katika kipindi cha mwaka 2020 hadi 2024, kumekuwa na ongezeko la uadilifu kwa watumishi wa umma.
“Pia, huwa tunapima kwa kuangalia mala-lamiko ambayo huwa tunayapokea kutoka kwa wananchi, kwamba, malalamiko hayo pia yamepungua, kwa hiyo kila mwaka yanapungua, mwaka 2020 yalikuwa mengi, 2021 yalipungua kidogo, mpaka sasa hivi yamepungua sana,” amesema Jaji Mwangesi.
Kamishna huyo wa Maadili amesema malalamiko mengi wanayoyapokea ni viongozi kutumia vibaya madaraka kwa kuwanyanyasa na kuwanyima haki zao, na kwamba yamepungua kutokana na elimu ya maadili wanayoitoa.
“Tunaamini kwamba kupungua huko kuna-tokana na elimu ambayo viongozi wamekuwa wakipata kutoka kwa maofisa wa sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma,” amesema Jaji Mwangesi.
Ameongeza kuwa mikakati ambayo wameiweka sas ni kuendelea kutoa elimu kwa kushirikiana na wadau wengine kama vyuo ili kuunganisha nguvu katika kutoa mafunzo ya maadili, hadi sasa wanakami-lisha awamu ya kwanza ya mafunzo hayo.
Kuhusu ujazaji wa matamko, Jaji Mwangesi amesema ni kosa kisheria kwa mtumishi wa umma kutojaza tamko la maadili na kuna hatua za kisheria ambazo huwa zinachukuliwa ikiwa ni pamoja na kupeleka mashauri Baraza la Maadili ambalo linasikiliza na kufanya uamuzi.
“Tunawapeleka kwenye Baraza, ambalo ni kama mahakama ya uadilifu, anapelekwa huko. Kama atakuwa na hatia, Baraza li-tamsikiliza, kama litamkuta na hatia, atati-wa hatiani na kuna taratibu ambazo huwa zinafuata baada ya hapo,” amesema.
Awali, akifungua warsha hiyo, jaji Mwangesi amesema kwa sasa wanapokea matamko ya Viongozi wa Umma kwa njia ya mtandao yaani Online Declaration Sys-tem (ODS). Amesema Sera ya Serikali Mtandao (e-Government) ambayo Serikali imeagiza Wizara, Idara na Taasisi zote za Umma kutumia mifumo ya Tehama katika kurahisisha mawasiliano na utendaji kazi Serikalini.
“Matumizi ya ODS ni hatua kubwa katika safari yetu ya maboresho na ubunifu wa ki-digitali wa kujenga mifumo ya kuwajali wadau wetu kwa kuwapunguzia adha ya kutumia gharama kubwa na muda mwingi kuwasilisha Tamko la Rasilimali na Mad-eni,” amesema.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kisheria wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Emma Ge-lani amesema Baraza la Maadili linafanya kazi zake kwa kutumia kanuni za mwaka 2007 ambazo zinaelekeza namna ya kufiki-sha malalamiko kwenye Baraza na Baraza kuyasikiliza na kuchukua hatua.
Amesema makossa ya maadili yako mengi kama yalivyoainishwa kwenye kifungu cha 6 na 12 cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, anapokiuka hapo basi atakuwa amevunja sheria na atafikishwa mbele ya Baraza.
“Kiongozi akifanya kazi kwa kupendelea, asipofuata sheria, kanuni na taratibu, akifanya matumizi mabaya ya mali ya um-ma, hayo yote ni makossa ya kimaadili am-bayo mtu anaweza kukiuka,” amesema mwanasheria huyo.
Ameongeza kuwa adhabu ambazo zimeain-ishwa kwenye sheria ni pamoja na kupewa onyo, kushushwa cheo, kufukuzwa kazi, kushauriwa kujiuzulu au kuchukuliwa hatua nyingine zozote kwa mujibu wa sheria za nchi.
“Kwa mwaka uliopita, 2024, Baraza lime-sikiliza mashauri 10 ya viongozi na hatua mbalimbali zilichukuliwa kulingana na kosa la mhuska,” amesema Gelani wakati aki-zungumza na waandishi wa habari.