Polisi yasubiri maelezo ya Padri Kitima sakata kushambuliwa kwake

Dar es Salaam. Ikiwa imepita mwezi mmoja tangu Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu (TEC), Padri Kitima ashumbuliwe, Jeshi la Polisi limeeleza hatua ilipofikia katika kufuatilia uchunguzi wa tukio hilo.

Padri Kitima alishambuliwa Aprili 30, 2025, majira ya saa nne usiku, katika makazi na Makao Makuu ya Baraza hilo yaliyopo Kurasini Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam. 

Katika tukio hilo, Padri Kitima inadaiwa alishambuliwa kwa kupigwa na kitu butu kichwani na tayari watu wawili wameshakamatwa wakidaiwa kuhusika na tukio hilo akiwemo Edward Cosseny (51) mkazi wa Dodoma na Mbezi Beach Makonde, Dar es Salaam, kufuatia chapisho lake la vitisho dhidi ya Padri Charles Kitima ambalo kwa mujibu wa ufuatiliaji alilitoa na kulichapisha mitandaoni siku chache kabla ya kutokea tukio lilomuhusisha Padri Kitima.

Akizungumza leo Jumamosi Mei 31, 2025 na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro kuhusu hali ya matukio mbalimbali ya kiuhalifu yaliyotokea kwa miezi miwili jijini humo, pia aligusia suala la Padri Kitima na hatua walioyofikia.

Kamanda Muliro amesema ni jukumu la kisheria kuhakikisha wanapata maelezo ya Padri kitima ya kimaandishi.

Kamanda Muliro amesema wakati ule tukio lilipotokea ilikuwa vigumu mtu akiwa anaumwa ukaanza kutumia njia ya kutaka kupata maelezo kutoka kwake.

Related Posts