Hekaya za Mlevi: Viongozi waige uadilifu wa nyuki
Dar es Salaam. Nyuki ni mdudu wa ajabu sana. Kwanza ana mbawa ndogo kulinganisha na mwili wake. Inashangaza jinsi anavyoweza kuzitumia mbawa hizo kuubeba na kusafirisha angani mwili wake mzito. Akiwa nchi kavu na angani hukutana na misukosuko ya ndege, mijusi na vyura wanaomwinda kwa ajili ya kitoweo. Kwa bahati nyuki ameumbwa akiwa na rangi kali…