Vibaka tishio Arusha, wadaiwa kumuua dereva wa lori akitafuta gesti
Arusha. Wimbi la uhalifu, hususan linalotekelezwa na makundi ya vijana wa mitaani maarufu kama vibaka, limeendelea kuwa tishio katika Jiji la Arusha, ambapo tukio la hivi karibuni limemgusa mtu aliyedaiwa kutambuliwa kuwa dereva wa lori, Maulid Rajabu (35), kudaiwa kuuawa kwa kuchomwa visu na kisha kutupwa pembezoni mwa barabara na watu wanaodaiwa kuwa vibaka. Mauaji…