Boni yai amtaka Mbowe asiwe mnyonge, akumbushia mchango wake

Hai. Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani wa Chadema, Boniphace Jacob, maarufu Boni Yai amesema kazi iliyofanywa na Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho,  Freeman Mbowe  kwa miaka 21 wanaithamini na kumtaka asikae pembeni kwa kuwa bado wanamuhitaji na wataendelea kumlinda. Bon Yai ameyasema hayo leo Alhamisi Mei 29, 2025 wakati akizungumza na  wananchi kwenye mkutano wa…

Read More

Fumbo la Samia, nani wa kuipasua CCM?

Dodoma. Kauli ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan juu ya ‘wenye dhamira ya kukipasua chama hicho’ imekuwa kama fumbo ambalo limewaacha wanachama wa chama hicho na tafakuri tofauti, kila mmoja akiichambua kivyake. Aidha, kauli hiyo imeelezwa na wasomi wa sayansi ya siasa kuwa inaashiria kwamba ndani hakuko shwari. Rais Samia…

Read More

Wakulima walalamikia mizani feki zao la pamba

Shinyanga. Baadhi ya wakulima wa zao la pamba mkoani Shinyanga wametoa sababu inayowazuia kusajili biashara zao katika mfumo wa ununuzi na uuzaji ni matumizi ya mizani feki kwa wanunuzi ambayo inawasababishia hasara. Hayo yamebainishwa leo Mei 29, 2025 katika mkutano wa wakulima wa zao la pamba, kampuni ya ununuzi, pamoja na vyama vya ushirika wa…

Read More

Takukuru yafanya ukaguzi wa maeneo ya wazi yaliyovamiwa

Morogoro. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na wataalamu wa ofisi ya Mkurugenzi imefanya ukaguzi wa maeneo yote ya wazi yaliyovamiwa na kuendelezwa na wawekezaji, ili kufanya tathimini ya kina kuhusu uwekezaji uliofanyika ili kubaini kiasi cha upotevu wa fedha za mapato. Akitoa taarifa hiyo kwa niaba ya…

Read More

Mwongozo wa hedhi kuleta ahueni kwa wasichana Tanzania

Dodoma. Serikali imezindua Mwongozo Taifa wa Afya na Usafi wa Hedhi wa mwaka 2025, utakaowezesha shule na maeneo ya kijamii kutenga vyumba maalumu kwa ajili ya wanawake kujistiri wakati wa hedhi, huku Serikali ikigharamia pedi mashuleni. Hatua hiyo imekuja ikiwa imepita miaka minane tangu kuwe na hekaheka za kampeni mbalimbali za kutaka taulo za kike…

Read More

Kocha Geita aikubali Stand United

Kocha wa Geita Gold FC, Mohamed Muya amewapongeza vijana wake na wa Stand United, huku akisema mikakati yake ya sasa ni kurekebisha makosa yaliyojitokeza katika kikosi chao. Muya ameyasema hayo alipozungumza na waandishi wa habari leo Mei 29, 2025 baada ya kumalizika kwa mechi ya marudiano ya play off kuwania kupanda Ligi Kuu Bara msimu…

Read More

15 Mbaroni tuhuma za wizi wa miundombinu ya barabara

Tabora: Jeshi la Polisi mkoani Tabora linawashikilia watu 15 kwa tuhuma za wizi wa taa za barabarani, sola paneli na betri za sola  katika barabara ya Tabora kwenda mkoani Katavi. Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 29,2025 Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Tabora,  Richard Abwao amesema watuhumiwa hao wamekamatwa katika msako mkali uliofanywa mkoani…

Read More

Wadau wakutana kujadili mifumo endelevu ya chakula

Arusha. Wadau kutoka taasisi za Serikali, mashirika ya umoja wa mataifa, sekta binafsi wamekutana kwa siku mbili jijini Arsuaha katika warsha ya kujadili namna ya kuboresha mifumo ya chakula nchini. Wadau hao wamekutana kuanzia leo Alhamisi Mei 29, 2025 ambapo pamoja na masuala mengine watajadili namna ya kuongeza uelewa wa kina wa mifumo ya chakula…

Read More