Sakata la RC na kadi za mpigakura latinga barazani, Serikali yajibu
Unguja. Sakata la Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Idrisa Kitwana, kuwataka wafanyakazi wa Serikali mkoani kwake wawasilishe kadi zao za mpigakura azikague, limeibukia Baraza la Wawakilishi, wakitaka kujua maagizo hayo aliyatoa wapi kwa sababu yanavunja sheria za nchi. Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais leo Alhamisi…