Bunge lapokea pongezi za Simba, Yanga katika viwango vya ubora

 Serikali imezimwagia sifa klabu za Simba na Yanga kwa kuendelea kuiwakilisha nchi katika mashindano makubwa barani Afrika. Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Profesa Palamagamba Kabudi ambaye amesema juhudi za klabu hivyo zimewezesha ligi ya Tanzania kushika nafasi ya nne kwa ubora Afrika. Profesa Kabudi ametoa kauli hiyo Bungeni leo…

Read More

Sh43 milioni za AHF kuimarisha udhibiti maambukizi ya Ukimwi

Musoma. Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na mapambano dhidi ya Ukimwi, Healthcare Foundation (AHF), limekabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh43 milioni kwa ajili ya kuimarisha juhudi za kudhibiti maambukizi ya Ukimwi katika Mkoa wa Mara. Msaada huo unaojumuisha pikipiki, kompyuta, printa, simu za mkononi, luninga na vifaa vingine, umetolewa kwa…

Read More

Chombo cha kusimamia miundombinu ya michezo kuanzishwa

Serikali imeanza mchakato wa kuanzisha chombo maalumu cha usimamizi wa miundombinu ya michezo katika kukabiliana na changamoto za uendeshaji wa miundombinu ya michezo nchini. Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi leo Mei 7, 2025 wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara yake kwa mwaka 2025/26. Profesa…

Read More

Mfumo wa malipo waliza watumishi wa umma, wawakilishi waingilia kati

Unguja. Licha ya Serikali kuanzisha Mfumo Jumuishi wa Taarifa za Utumishi na mishahara ili kuboresha utendaji na kupata takwimu sahihi za wanaolipwa mishahara, umetajwa kukabiliwa na changamoto huku ukiwalipa watumishi wa umma mishahara pungufu na kuzua taharuki. Wawakilishi wa Baraza la Wawakilishi wameitaka Serikali kuangalia namna ya kufanya marekebisho na kuubadilisha. Wamesema kitendo cha kuwapatia…

Read More

Badru awataka watumishi wa umma kuchangamkia fursa ya uwekezaji WHI

Na Mwandishi wetu MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Watumishi Housing Investment (WHI), AbdulRazak Badru ametoa wito kwa watumishi wa Umma kuchangamkia fursa ya uwekezaji kupitia dirisha E-Wekeza linalotarajiwa kuzinduliwa na serikali kupitia mfumo wa watumishi portal hivi karibuni.  Badru ameyasema hayo wakati akizungumza na wawekezaji na wajumbe wa bodi katika Mkutano Mkuu…

Read More

Uzembe wa madereva watajwa sababu ajali nyingi, wao wabainisha mambo matatu

Dar es Salaam. Uzembe wa madereva wa vyombo vya moto nchini umetajwa kuwa sababu iliyobeba asilimia 44.1 ya ajali zote zilizotokea mwaka 2024, hali iliyochangia kuongezeka kwa idadi ya waliopoteza maisha. Wakati wao wakinyoshewa kidole, madereva wamesema hawapaswi kulaumiwa moja kwa moja, kwani hadi ajali inapotokea huwa kuna sehemu tatu zinazosababisha, ikiwamo upande wa dereva…

Read More