TANZANIA YAENDELEA KUSHIRIKIANA NA NCHI WASHIRIKA KUKABILIANA NA UJANGILI
Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii itaendelea kushirikiana na Nchi Wanachama wa Mkataba wa Lusaka katika kukabiliana na biashara haramu ya Wanyamapori na mazao ya misitu inayovuka mipaka ya Nchi ili kuboresha uhifadhi, kuendeleza utalii na kukuza uchumi. Akifungua Mkutano wa 14 wa Kamati ya Wataalam wa Baraza la Usimamizi wa Mkataba wa Lusaka…