Mambo sita kuboresha sekta ya elimu

Katavi. Wakati Tanzania ikiungana na mataifa mengine kuadhimisha juma la elimu, wadau wa elimu wamependekeza mambo kadhaa kufanyika kwenye sekta hiyo ikiwemo kuwekeza katika elimu inayolenga kujenga uwezo na stadi za maisha kwa vijana. Wadau hao ambao wamekusanyika katika Halmashauri ya Mpimbwe mkoani Katavi wakiadhimisha juma hilo wamesema Tanzania inahitaji mfumo wa elimu unaompa kijana…

Read More

Wabunge walia na madeni ya makandarasi, fidia

Dodoma. Wabunge wameitaka Serikali kuandaa mkakati maalumu wa kulipa madeni ya makandarasi na wahandisi washauri, huku Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ikisema hadi kufikia Februari 2025 deni limefikia Sh1.29 trilioni. Wameyasema hayo wakati wakichangia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi wa wizara hiyo kwa mwaka 2025/26 bungeni leo Jumatatu Mei 5, 2025….

Read More

Mkunga ataja faida kujifungulia kwenye maji

Shinganya. Mwanzilishi wa huduma ya kujifungulia kwenye maji Taifa, mkunga mtaalamu Agnes Ndunguru ameeleza faida ambazo humsaidia mama anayejifungua kwenye maji pamoja na mtoto, wakati huduma hii inapotimiza miaka mitatu tangu kuanzishwa nchini. Akizungumza leo Jumatatu Mei 05, 2025 mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha katika maadhimisho ya siku ya wakunga duniani…

Read More

Tamisemi yataka kata ya Mabogini kugawanywa

Moshi. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa ameelekeza kuanza kwa mchakato wa kugawanywa kwa kata ya Mabogini, yenye watu zaidi ya 60,000 iliyopo wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro. Kugawanywa kwa kata hiyo, kunatokana na idadi kubwa ya watu wanaoishi eneo hilo, ambapo pamoja na mambo…

Read More