Ubunge wa Siha unavyomtesa Dk Mollel, awalalamikia Takukuru
Siha. Mbunge wa Siha mkoani Kilimanjaro, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel ameibua gumzo wilayani humo, akituhumu kuhujumiwa ubunge wake huku akivihusisha vyombo vya usalama ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), ambapo taasisi hiyo imejibu hoja hiyo. Siyo mara ya kwanza Dk Mollel kulalamika kuhujumiwa ubunge wake, mara…