KONA YA MZAZI: Tusiwaharibu watoto kwa hoja ya kulinda haki za binadamu
Katika hali kama hii, wazazi wameachwa na jukumu kubwa na gumu zaidi la kulea watoto katika njia ya haki na kuwaepusha na maangamizi ya kimaadili, kijamii na kisaikolojia. Hali halisi inayotokea kwenye jamii zetu kama mzazi kumpiga mtoto kwa nia ya kumrekebisha, jirani kuingilia na kuleta tafrani, inaonesha jinsi malezi yalivyopoteza dira na mshikamano wake…