Kauli ya RC Kitwana yazua mjadala
Unguja. Siku chache baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Idrissa Kitwana kuwataka watendaji wa Serikali waliopo chini yake kuwasilisha kadi zao za mpigakura azikague, wadau wa uchaguzi wamesema hatua hiyo ni kuingilia majukumu ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC). Pia, wamesema inalenga kutoa vitisho na kuwapa hofu watumishi wa umma na kuwaelekeza nini…